Kundi la Taliban lateka mji wa Sangin nchini Afghanistan

Kundi la Taliban lateka mji wa Sangin nchini Afghanistan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la Taliban lateka mji wa Sangin nchini Afghanistan

Kundi la Taliban limeteka mji muhimu ulio kusini mwa Afghanistan wa Sangin baada ya mapigano yaliyodumu kipindi chama mwaka mmoja

Msemaji wa gavana wa mkoa wa Helmand alithibitisha kuwa kituo cha polisi cha wilaya na makao makuu ya gavana sasa viko mikononi mwa Taliban.

Karibu robo ya wanajeshi wa Uingereza waliuawa wakati wa oparesheni ya kijeshi ya Uingezrea nchini Afghanistan walipokuwa wakiulinda mji wa Sangin.

Mamia ya wanajeshi wa Afghanistanwameuwa hivi majuzi wakati wa mapigano.

Nao takriban polisi 9 waliuawa katika eneo la kunduz mapema siku ya Alhamisi.

Mlinzi ambaye maafisa wanasema alikuwa na uhusiano na Talibana, aliwaruhusu wanamgambo hao kuingia ambapo pia wanaripotiwa kuondoka na silaha.

Image caption Kundi la Taliban lateka mji wa Sangin nchini Afghanistan

Taliban tayari inadhibiti maeneo makubwa ya Helmand lakini kutekwa kwa mji wa Sangin, inaonyesha changamoto zinazoikumba serikali na washirka wake wa nchi magharibi.

Kutekwa kwa mji wa Sangin na ishara ya kuzidi kukua kwa Taliban maeneo ya Kusini.

Msemaji wa Taliban Qari Yousuf Ahmadi anasema kuwa wanamgambo waliteka mji huo na sehemu muhimu. Wapiganajai wa Taliban tayari wamezingira makao ya wilaya.

Msemaji wa jeshi la Afghanistan alisema kuwa wanajeshi walikuwa wameondolewa na kupelekwa kambini kuafuatia amri kutoka kwa mkuu wa majeshi.

Ripoti zinasema kuwa vikosi vya kigeni vimeanza kushambulia eneo hilo, ambalo limeshuhudia mapigano kwa zaidi ya miaka kumi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kundi la Taliban lateka mji wa Sangin nchini Afghanistan

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii