Polisi A. Kusini waonya juu ya teksi za wabakaji mjini Johannesburg

Teksi za mabasi madogo mjini Johannesburg Haki miliki ya picha AFP
Image caption Teksi za mabasi madogo hutumiwa kwa kiasi kikubwa kwa safari za umma mjini Johannesburg

Mvulana wa miaka 10 alilazimishwa kulala kifudi fudi wakati mama yake akibakwa kwa muda wa saa nne katika teksi mjini Johannesburg , kwa mujibu wa ripoti kutoka Afrika kusini.

Yeye na mama yake wanadaiwa kulaghaiwa kuingia ndani ya teksi ya basi dogo kabla ya kufanyiwa maasi hayo na kuamrishwa kukabishi kadi yake ya benki pamoja na namba za siri(PIN) za kadi ya benki Pna wanaume watatu waliokuwa wamejihami kwa bunduki

Inadhaniwa kuwa kuwa hili lilikuwa ni shambulio la hivi karibuni la genge la majambazi.

Taarifa za kwanza za "teksi za ubakaji " zilitolewa mwaka mmoja uliopita.

kwa mujibu wa rekodi za Roodeport, mashambulio ya awali ya ubakaji yaliripotiwa mwezi Machi 2016, huku mashambulio matatu yakifanyika katika kipindi cha wiki ya mwisho ya mwezi Juni.

Matukio yote yalifanyika ndani ama karibu na kitongoji cha Soweto mjini Johannesburg.

hata hivyo haijjabainika wazi ni mashambulio mangapi yaliyokwisha tokea huko katika kipindi cha miezi 12, ama ikiwa yote yalitekelezwa na genge hilo hilo.

Luteni kanali Lungelo Dlamini ameiambia BBC: "Kikundi cha wanaume watatu ama wawili waliokuwa wakiendesha magari mawili tofauti ya [Toyota] Quantums, moja la rangi ya majivu na jingine la rangi nyeupe, yali wachukua wanawake wawili yakijifanya ni magari ya teksi, wakawapora kwa silaha na baadae kuwabaka."

Bwana Dlamini amesema kuwa haijabainika wazi kuwa magari hayo ya Quantum yalikuwa yana njama moja ama kila moja lilikuwa linatekeleza uhalifu huo kivyake

Hadi sasa, wanawake wawili -akiwemo mama wa mvulana huyo -wamekwisha zungumza na vyombo vya habari vya Afrika Kusini, kuelezea kilicho wasibu.

Mwanamke wa pili alikiambia kituo cha redio cha Kaya FM namna mwanamume aliyempata baada ya kushambuliwa aliwasaidia wanawake wengine wanaodhaniwa kubakwa katika eneo hilo hilo .

Amesema genge hilo limekuwa likiendesha uhalifu huo, kulingana mtandao wa habari wa -Afrika News network.

Wanawake wote wawili walichukuliwa nyakati za mchana.

Baada ya mama na mwanae kuingia ndani ya teksi, mvulana alilazimishwa kulala kifudi fudi chini kwenye sakafu ya gari hilo, huku wanaume watatu wakimbaka mama yake.

Muathiriwa huyo aliliambia shirika la habari la EyeWitness News kwamba alikuwa anaomba wakati wa tukio hilo majangili wasimuumize mwanae.

Afrika Kusini ina viwango vya juu vya visa vya ubakaji vinavyoripotiwa duniani.