Mtu mmoja akamatwa kwa kuendesha gari kwa umati Ubelgiji

Gari hio lilisimamishwa na polisi wa kutoa huduma za dharura Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari hio lilisimamishwa na polisi wa kutoa huduma za dharura

Raia wa Ufaransa mwenye asili ya nchi za Kaskazini mwa Afrika, amekamatwa kwenye mji wa Antwerp nchini Ubelgiji, kwa kushukiwa kuendesha gari kuenda kwa umati wa watu.

Gari liliendeshwa kwa kasi eneo la De Meir ambao ni mtaa wenye shughuli nyingi wa mji wa Atwerp, kabla ya kusimamishwa. Hakukuwa an ripoti za majeraha yoyote.

Visu, bunduki na bidhaa za maji maji ambavyo havikutambuliwa vilikuwa ndani ya gari hilo.

Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amepongeza mamlaka kwa kazi yao nzuri.

shambulizi hilo linakuja siku moja baada ya gari kuendeshwa kwa kasi jijini London na kuwagonga watu wengi kabla ya dereva kutoka nje na kungia kwenye uwanja vya majengo ya bunge.

Aliuawa baada ya kumchoma kisu vibaya afisa wa polisi. Watu wengine wawili waliuawa na wengine 40 kujeruhiwa.

Ilikuwa pia siku ambapo ubelgiji ilikuwa inaadhimisha mwaka mmoja tangu mashambulizi mawili ya bomu kuwau watu 32 mjini Brussels.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gari hio lilisimamishwa na polisi wa kutoa huduma za dharura