Michezo ya kufuzu kombe la dunia leo

KOMBE LA DUNIA Haki miliki ya picha Google
Image caption Neno ya kombe la dunia la mwaka 2018 michuano itayofanyika nchini Urusi

Nyasi za viwanja tisa zitawaka moto leo katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia la mwaka 2018 kwa kanda ya ulaya.

Michezo ya kundi D Georgia watacheza na Serbia, Austria watakua wenyeji wa Moldova na Ireland wakicheza na Wales.

Katika kundi G Hispania watakipiga na Israel, Liechtenstein wao watapimana ubavu na Macedonia, waitaliano wao watakipiga na Albania.

Croatia wao watakua wenyeji wa Ukraine, huku Kosovo wakicheza na Iceland nao Finland wakiwa ugenini dhidi ya Uturuki hii ikiwa ni michezo ya kundi I