Matokeo ya michezo ya kirafiki

Nigeri vs Senegal Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cheikh Ndoye wa Senegal kushoto akikabiliana na Ogenyi wa Nigeria

Miamba wa soka wa Afrika Nigeria na Senegal wakicheza mchezo wao wa kirafiki nchini England walikwenda Sare ya kufungana 1-1.

Majirani wa ukanda wa Afrika Mashariki timu ya Uganda The Cranes na kenya The Harambe Stars pia walishindwa kutambiana baada ya kwenda sare ya 1-1.

Jordan wakiwa nyumbani wakashinda kwa ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Hong Kong, Afghanistan wao wakawachapa Singapore kwa 2-1.

Bahrain wakashindwa kutamba nyumbani kwa kukubalia sare ya 1-1 na Tajikistan