London:Idadi ya waliokufa yaongezeka

Mzee mmoja wa miaka 75 aliyekuwa miongoni mwa waliojeruhiwa amefariki dunia Haki miliki ya picha AP
Image caption Mzee mmoja wa miaka 75 aliyekuwa miongoni mwa waliojeruhiwa amefariki dunia

Idadi ya watu waliouawa wakati wa shambulio nje ya Bunge jijini London siku ya jumatano imeongezeka na kufikia wanne baada ya kifo cha mzee wa miaka 75.

Alikuwa mmoja kati ya watu kadhaa waliojeruhiwa gari ilipovurumishwa na kugonga watu kwenye daraja la Westminster.

Polisi wamesema watu wanane wamekamatwa wakihusishwa na mauaji , wanashikiliwa wakishukiwa kupanga mashambulio ya kigaidi.

Mamia ya asakri wanafanya msako jijini London, Birmingham na Wales.

Mshambuliaji Khalid Masood waliuawa na Polisi.

Maelfu ya watu wamehudhuria ibada katikati mwa London kuwakumbuka waathiriwa.