Rais wa zamani wa Argentina kufikishwa mahakamani

Bi Cristina Fernandez amesema kuwa anaandamwa kisiasa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bi Cristina Fernandez amesema kuwa anaandamwa kisiasa

Jaji wa Mahakama nchini Argentina ameamuru kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Cristina Fernandez de Kirchner kusimama kizimbani ili kusikiliza mashtaka dhidi yake ya matumizi mabaya ya fedha.

Fernandez na maafisa wengine 13 akiwemo waziri wa zamani wa uchumi na aliyekuwa Mkuu wa Benki kuu Argentina wameshutumiwa, kuiamuru Benki kuuza deni la serikali, ili kulilipa kwa gharama ndogo.

Mwendesha mashtaka amesema hatua hiyo imeikosesha Argentina mamilioni ya dola.

Bi Fernandez amekana kufanya makosa na kusema kuwa Kesi hiyo ina ushawishi wa kisiasa.

Fernandez ambaye alikuwa rais wa kuanzia mwaka 2007 mpaka mwaka 2015 amekuwa akihusishwa na vitendo vya rushwa na anafanyiwa uchunguzi kuhusu shutuma nyingine.