Picha bora Afrika : Kati ya tarehe 17 na 24 Machi, 2017

Mkusanyiko wa picha bora kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika na Waafrika katika maeneo mbali mbali ya Afrika wiki hii

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashindano siku ya Jumanne wakati wa tamasha la kitamaduni la mwaka la Ingomainayochezwa na watu wa kabila la Zulu mjini Durban, Afrika Kusini...
Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Shindano hilo linajumuisha uimbaji..
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Na hucheza
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku hiyo hiyo katika wilaya ya Muhanga Muhanga, kusini mwa Rwanda, ndege isiyokuwa na rubani ikitupa furushi la damula a drone releases a blood package during the visit of World Bank head Jim Yong Kim.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Siku ya Jumatano watoto wakishiriki katika uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa yambio za ngamia katika jangwa la Sarabium Ismailia, Misri...
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ayman, mmoja wa wavulana wanaoshiriki mbio za ngamia, akionyesha upendo kwa ngamia wake muda mfupi kabla ya mbio hizo kuanza.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakati huo huo, waendesha baiskeli walishiriki mashindano ya baiskeli eneo la Greyton, Afrika kusini , huku helikopta ikizunguka juu yao kufuatilia mashindano hayo
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumapili, watoro wa Tunisiawakishiriki katika ''matembezi ya maua'' mjini Tunis, tmji mkuu, kuonyesha haki ya utamaduni wao na haki ya kulindwa na hatari ya ugaidi.
Haki miliki ya picha AHMED JALLANZO
Image caption Shabiki akionyesha ushabiki wake kwa timu ya Liberia BYC walipokuwa wakicheza mechi Jumapili dhidi ya Ferroviario da Beira kutoka Msumbiji.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Boris Johnson akiwa ziarani nchini Ethiopia alipata fursa ya kujima uwezo wake wa mbio kwa kukimbia na Haile Gebrselassie, mkimbiaji mashuhuri wa mbio za masafa marefu...
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pia alitumia fursa hiyo kuangalia ya mifupa ya mwili wa mmoja wa binadamu walioishi kale zaidi iliyokarabatiwa anayefahamika kama Lucy.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katika shughuli za wiki, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari siku ya Jumatano alipata muda walau wa kushiriki maombi wakati wa mkutano wa viongozi wa wakuu mjini Abuja.
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku ya Jumatano , wafanyakazi mjini Cape Town waliweka picha kubwa ya Askofu Desmond Tutu, mshindi wa tuzo ya amani ya nobel, kama sehemu ya kuadhimisha kujitolea kwake katika masuala ya kijamii.

Mada zinazohusiana