Okocha amsifu mchezaji wa Kenya Victor Wanyama

Aliyekuwa mshambuliaji wa Nigeria na Bolton Wanderers Jay Jay Okocha anasema kuwa idadi ya juu ya wachezaji wa Kenya barani Ulaya itaipiga jeki timu ya taifa hilo
Image caption Aliyekuwa mshambuliaji wa Nigeria na Bolton Wanderers Jay Jay Okocha anasema kuwa idadi ya juu ya wachezaji wa Kenya barani Ulaya itaipiga jeki timu ya taifa hilo

Aliyekuwa mshambuliaji wa Nigeria na Bolton Wanderers Jay Jay Okocha anasema kuwa idadi ya juu ya wachezaji wa Kenya barani Ulaya itaipiga jeki timu ya taifa ya harambee stars na kuwa na mchezo mzuri.

Kulingana na runinga ya NTV nchini Kenya Okocha amesema kuwa mchezaji wa Kenya Victor Wanyama anayechezea soka yake ya kulipwa katika klabu ya Tottenham nchini Uingereza anaifanyia kazi nzuri Kenya na bara la Afrika.

''wakati wachezaji wetu wanapofanya vizuri kule Ulaya hawasemi kwamba ni mchezaji wa Kenya,wao husema mtazameni yule mchezaji kutoka Afrika, lakini twashukuru kwamba wanyama anafanya kazi nzuru sana''

Image caption Mchezaji wa Kenya anayeichezea klabu ya Tottenham Victor Wanyama akimchenga Sadio Mane wa Liverpool

Okocha amesema kuwa ni vyema kwamba mchezaji huyo anaipeperusha bendera ya Kenya juu na kwamba hatua hiyo inafaa kuwafungulia milango wachezaji zaidi wa Kenya kwenda Ulaya.

Amesema kuwa shirikisho la soka la Kenya linafaa kuchukua hatua mwafaka kwa lengo la kutumia fursa hiyo ili kuwasaidia vijana zaida kujiunga na klabu za Ulaya.