Gari la Uber linalojiendesha lahusika katika ajali Marekani

Magari ya UBER
Image caption Magari ya UBER

Gari moja linalojiendesha kutoka kampuni ya Uber limepata ajali kwa kugongana na gari lingine huko nchini Marekani katika jimbo la Arizona,

Picha zimeonyesha gari hilo likiwa limepinduka lakini bado hakuna taarifa zozote za majeruhi.

Kituo kimoja cha televisheni kimeripoti kuwa dereva wa gari lililohusika katika ajali na gari la Uber hakuipisha gari hiyo.

Hatahivyo haijulikani iwapo gari hilo la Uber lilikuwa kwenye mfumo wa kuendeshwa bila dereva au la .

Huduma hiyo ya kampuni ya Uber ya magari yanayojiendesha bila dereva ilianza safari zake za uchukuzi mjini Arizona mwezi uliopita, ikiongeza uchukuzi wa safari hiyo kwenye miji mengine kama vile Pittsburgh na San Francisco.

Huwezi kusikiliza tena
Madereva wa Uber wameandamana kupinga punguzo la bei

Kampuni za kiteknologia zinafanya harakakti za kuboresha huduma hiyo ya usafiri wa magari yasiyo na madereva kwa lengo la kumiliki biashara hiyo ambayo thamani yake inakadiriwa kukuwa na kufikia bilioni ishirini katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Mada zinazohusiana