Vita dhidi ya Polio vyapelekwa Afrika Magharibi na kati

WHO ndilo linaloendeleza kampeni hiyo kubwa ya kuwapatia chanjo hiyo dhidi ya maradhi ya polio watoto wote walio chini ya umri wa miaka 5 katika mataifa ya Afrika magharibi na
Image caption WHO ndilo linaloendeleza kampeni hiyo kubwa ya kuwapatia chanjo hiyo dhidi ya maradhi ya polio watoto wote walio chini ya umri wa miaka 5 katika mataifa ya Afrika magharibi na

Kikosi kikubwa cha wafanyikazi wa afya katika nchi za Afrika ya kati na Afrika magharibi leo kinaanza harakati za kuwapa chanjo watoto zaidi ya laki millioni katika jitihada za kutokomeza baadhi ya polio inayokumba baadhi ya maeneo kama vile kazkazini mashariki mwa Nigeria.

Shirika la afya duniani WHO ndilo linaloendeleza kampeni hiyo kubwa ya kuwapatia chanjo hiyo dhidi ya maradhi ya polio watoto wote walio chini ya umri wa miaka 5 katika mataifa ya Afrika magharibi na kati wakilenga hasa ukanda wa kutoka Mali hadi Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo kwenye kipindi cha siku nne tu.

Tishio la kuenea kwa maradhi ya polio yanayosababisha kupooza imechochewa na hali ya watu wengi kuyakimbia makaazi yao kwa sababu ya mashambulio ya makundi kama vile Boko Haram, hivyo raia kutofikiwa na huduma za chanjo.

Viini vya maradhi ya polio husambaa kwa kasi , huathiri zaidi watoto na kusababisha ulemavu wa maisha .

Huku ikiwa bado ni tisho zaidi katika mataifa ya Nigeria, Afghanistan na Pakistan.

Mada zinazohusiana