Mwanamitindo anayeugua 'ugonjwa wa paka'

Caitin Stickels Haki miliki ya picha caitinkitten

Mwanamitindo Caitin Stickels ana tatizo nadra sana la kiafya ambalo hufahamika kama 'Ugonjwa wa macho ya paka' ambalo humsababishia maumivu makali sana.

Lakini bado hajakata tamaa.

Tatizo hilo la kiafya humfanya aonekane kama paka.

Hali yake ilimvutia mpiga picha za mitindo kutoka Uingereza Nick Knight.

Alimtazama mwanamitindo huyo wa miaka 29 kutoka Seattle mara ya kwanza kwenye Instagram.

Tangu wakati huo, amevuma kama mwanamitindo na hata picha zake zikachapishwa katika jarida la V Magazine.

"Ni mabadiliko makubwa zaidi mema yaliyowahi kutokea katika maisha yangu," aliambia BBC.

Ugonjwa huo wa macho ya paka hufahamika kitaalamu kama Schmid-Fraccaro Syndrome.

Watu wenye ugonjwa huo wanaweza kuwa na matatizo katika maumbile ya masikio yao, moyo na kwenye figo.

Wakati mwingine, viungo vingine mwilini huathiriwa.

Sura ya Caitin si kama ya wanamitindo wengi ambao wamevuma sana.

'Urembo' wake si kama ule wengi waliozoea kuona ukiangaziwa kwenye majarida, filamu na runinga.

"Sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo au kufikiria ningeshiriki katika tasnia ya mitindo na mavazi," aliambia BBC.

Haki miliki ya picha Caitinkitten

'Watu waliniogopa'

"Mahangaiko mengi kwangu kutokana na ugonjwa huu huwa ni ndani ya moyo wangu," anasema.

"Nafikiri jambo jingine ni kwamba macho yangu huwa hawayumbuki kivyake; na hivyo hukaa kama ya paka wakati wote.

"Hii hata hivyo huniwezesha kuona vyema usiku, ninaweza nikatatizwa na jua kali. Nalipenda jua na mara nyingi hutokea nje na kutembea, lakini hilo hutatiza macho yangu."

Caitin anasema pia hupata maumivu makali mwilini na kupata kichefuchefu.

"Mwili wangu huathiriwa sana na mabadiliko katika mazingira, lakini kwa sababu umekuwa hivyo kwa muda mrefu, watu wengi niliotangamana nao huwa hawatambui kwamba kuna tatizo. Mimi ni mgumu kama jiwe."

"Kazi yangu ya uanamitindo, uigizaji na uimbaji hunisaidia sana kusahau maumivu niliyo nayo moyoni.

"Ni figo moja pekee yangu inayofanya kazi, kwa hivyo huwa inanibidi kunywa maji sana.

"Na sura yangu? Watoto wakati mwingine ndio hunishangaa. Lakini sana huwa sikabiliwi na unyanyapaa.

"Utoto wangu ulikuwa vile vile. Watoto ni watoto tu, ni kweli walinicheka na kunichezea. Lakini nani hakufanyiwa hivyo?"

"Sote huwa na kasoro pahala fulani na sote ni watu binafsi. Hakuna aliyekamilika," anaongeza.

Haki miliki ya picha caitinkitten

"Jambo moja ni kwamba sote hatufanani na hakuna asiye na doa pahali."

Haki miliki ya picha Caitinkitten
Haki miliki ya picha Caitinkitten

Mada zinazohusiana