Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha

Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha

Katika eneo moja mashariki mwa Zambia mwandishi wa BBC Chris Haslam, anakumbana na kijana mdogo ambaye anajikakamua kusukuma baiskeli kubwa ambayo imebeba mitungi ya maji, kuni na mfuko wa mchele.

Kwa vile kijana anaisukuma baiskeli hiyo na mikono yake miwili, hana njia ya kuwafukuza nzi kutoka kwa macho yake.

Jina lake ni "Mulangani". Jina hilo ni la jamii ya Nguni linalomaanisha "niadhibu" au yule ambaye ni lazima adhibiwe. Chris Haslam alimuuliza dereva kuhusu ni nani anayeweza kumpa mtota wake jina baya kama hilo?

"Labda babu yake au chifu," dereva akajibu. Nchini Zambia na hata Zimbabwehasa mashambani , ni jambo la kawaida wazazi kuwaalika wazee wa jamii kuwapa majina watoto wanapozaliwa.

Mara nyingine chifu huwa anataka kuiadhibu familia, anasema dereva, "au anafikiri kuwa mtoto aliyezaliwa ni mzigo kwa familia."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha

Lakini kijana huyo si peke yake aliye na jina la kutisha. Baadaye anakutana na "Chilumba", jina linalomaansiha "kaburi la ndugu yangu"

Kisha anakutana na Balaudye - "nitaliwa" na Chakufwa- "amekufa"

Pia anakutana na Daliso linalomaanisha "baraka" na Chikondi linalomaanisa "upendo".

Kwenye utamaduni wa Afrika kuna tabia ya kuwapa watoto majina kutokana na nyakati walizozaliwa, kwa mujibu wa Clare Mulkenga afisa wa huduma za watoto nchini Zambia.

Anasema kuwa hata hivyo ni vyema kwa wale wanaozaliwa nyakati nzuri lakini pia huwa ni bahati mbaya kwa wengine.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eneo ambapo watoto hupewa majina ya kustaajabisha