Waasi washikilia uwanja wa ndege Syria

Uharibifu uliofanywa na vita vinavyoendela Syria
Image caption Uharibifu uliofanywa na vita vinavyoendela Syria

Wapiganaji wanaowaunga mkono waasi nchini Syria wanasema kuwa wamedhibiti eneo muhimu la uwanja wa ndege ambalo awali lilikuwa likitumika na kundi la Islamic State karibu na mji wa Raqqa kabla ya kushikiliwa na serikali.

Kundi hilo la SDF limesema limeshikilia eneo la Tabqa, kilomita 40 Magharibi mwa Raqqa.

Image caption Awali uwanja huu ulikuwa ukishikiliwa na serikali

Saa chache kabla ya tukio hilo, kundi la IS lilisema kuwa bwawa la Tabqa ambalo ni kubwa zaidi nchini Syria, lipo hatarini kubomoka kutokana na mshambulizi ya anga yanayofanywa na vikosi vya Marekani.

IS wameongeza kuwa vitendo hivyo vinalenga kuwafanya wakaazi wa mji wa Raqqa kuuhama mji huo.

Lakini jeshi la Marekani linasema hawajalenga bwawa hilo.