Chama cha Merkel chapata ushindi mkubwa jimboni Ujerumani

Merkel amekuwa Kansela wa Ujerumani tokea mwaka 2005
Image caption Merkel amekuwa Kansela wa Ujerumani tokea mwaka 2005

Chama cha Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel cha Christian Democrats, kimepata ushindi mkubwa katika kura za majimbo kwenye mji wa Magharibi uitwao Saarland.

Matokeo ya awali yanaonyesha wamepata ushindi wa zaidi ya asilimia 40 ya kura zote, ikiwa ni alama tano zaidi ya kura walizopata uchaguzi uliopita.

Wapinzani wakuu chama cha Social Democrats wamepata asilimia 29, ikiwa ni asilimia chache zaidi tokea kuchagulikwa kwa kiongozi wao mkuu Martin Schulz.