Urusi: waandamana kupinga matumizi mabaya ya madaraka

Polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji
Image caption Polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji

Maelfu ya raia wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini Urusi wakiandamana kupinga kile wanachodai matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mkusanyiko mkubwa upo katika mji wa Moscow ambapo shinikizo ni kumtaka waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev kujiuzulu.

Wanaharakati wanasema kuwa hadi sasa watu 800 wanashikiliwa na Polisi.

Maandamano haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi ya yale yaliyowahi kutokea nchini Urusi kwa miaka mingi, ambapo wanadai kuwa waziri mkuu wao Dmitry Medvedev amekuwa akutumia fedha za umma

katika mambo yake binafsi kwa kujenga majumba kifahari, kununua boti za kifahari, mashamba ya mvinyo na jumba la kufugia bata.

Image caption Maandamano makubwa yalikuwa katika mji wa Moscow

Katika viunga vya Pushkin mjini Moscow, kuna kundi kubwa la waandamanaji waliokusanyika, mmoja wao amesema kuwa fedha za serikali zinaibiwa.

Marekani imeilaumu Urusi kwa hatua yake ya kuwashikilia mamia ya waandamaji kwa madai kuwa wanavuja haki dhidi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa haki za binadamu.