Mafuriko yahamisha maelfu Australia

Picha za rada zikionyesha mwenendo wa kimbunga hicho
Image caption Picha za rada zikionyesha mwenendo wa kimbunga hicho

Maelfu ya watu wamehama makazi yao katika mji wa Queensland Kaskazini Mashariki mwa Australia baada ya kimbunga kupiga eneo hilo.

Mawimbi yanatarajiwa kusababisha upepo mkali na kuyafanya yaruke mita nane zaidi ya sasa.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa zaidi ya watu elfu tatu wamehama makazi yao huku wengine takriban elfu mbili wakishauriwa kufanya hivyo na mamlaka.

Kimbunga Debbie kinatarajiwa kusababisha mafuriko katika baadhi ya sehemu za pwani ya nchi hiyo.