Aliyemfunga mbwa wake mdomo atupwa jela miaka 5

Caitlyn Haki miliki ya picha Charleston Animal Society

Mwanamume mmoja raia wa Marekani ambaye alifunga mbwa wake kwenye mdomo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

William Dodson, mwenye umri wa miaka 43, anasema alimfunga mbwa huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana. Ililazimu mbwa huyo kufanyiwa upasuaji mara kadha baada ya kupoteza sehemu ya ulimi wake.

Siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa, William Dodson pia alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, kwa mashtaka tofauti ya bunduki.

Haki miliki ya picha Charleston Animal Society

Vifungo hiyo viwili vitafuatana.

Kulingana na polisi William Dodson alimnunua mbwa hiyo kwa jina Caitlyn kwa dola 20.

Haki miliki ya picha Facebook/Charleston Animal Society
Image caption Caitlyn

Dodson, ambaye alikuwa huru kwa dhamana wakati huo, alimfunga mbwa huyo nje baada ya kumfunga mdomo wake mara tisa.

Lakini mbwa huo alifanikiwa kutoroka mwezi Mei mwaka 2015, na alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda barabarani.

Kamba aliyotumia kumfunga mbwa hiyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi wake, na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.

Haki miliki ya picha FACEBOOK/CHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Image caption Caitlyn

Wakati huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha ya akaunti yake na kuweka picha ya mbwa hiyo, kama njia ya kuonyesha uzalendo.

Wamekuwa wakichapisha taarifa jinsi mbwa huyo anavyoendelea katika kisa hicho kilichoangaziwa kimataifa.

Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi 15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia tofauti.

Haki miliki ya picha FACEBOOK/CHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Image caption Caitlyn