Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny afungwa jela siku 15

Alexei Navalny (kushoto) aliitisha maandamano kupinga ufisadi ndani ya serikali Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alexei Navalny (kushoto) aliitisha maandamano kupinga ufisadi ndani ya serikali

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, amehukumiwa kifungo cha siku 15 jela kwa kukiuka amri za polisi wakati wa maandamano makubwaa siku ya Jumapili.

Bwana Navalny alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliokamatwa kwa kuhusika kwenye mikutano kadha kote nchini.

Mahakama mjini Moscow mapema ilimpiga faini ya karibu dola 350 kwa kupanga maandamano yaliyoharamishwa.

Leo Jumatatu, serikali ya Urusi iliulaumu upinzani kwa kuchochea kuvunjwa kwa sheria na uchokozi.

"Baadhi ya vijana walilipwa kushiriki maandamano," msemaji wa polisi alisema.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi ya waandamanaji walibeba bata au mabango ya bata

Bwana Navalny baadaye alimshutumu tena Dmistry Medvedev kwa kuhusika kwenye ufisadi.

Bwana Navalny alifikishwa mahakamani ya kukamatwa siku ya Jumapili na kushinda korokoroni. Licha ya kukwepa kifungo kwenye mashtaka ya kwanza, alihukumi kifungo cha siku 15 jela kwa kumpuuza afisa wa polisi.

Wakili wa bwana Navalny Olga Mikhailova, aliliambia shirika la Reuters kuwa, aliitarajia hukumu kama hiyo na kuwa atakata rufaa.

Kabla ya hukumu kutolewa leo Jumatu, bwana Navalny mwenye umri wa miaka 40, aliandika kwenye mtandao wa akiwa mahakamani akisema , "Hello kila mmoja, ni kutoka mahakama ya Trerskoy. Wakati utawadia tutawaweka hukumuni."

Alidai kuwa bwana Medvede ndiye anastahili kushtakiwa kama mwandalizi mkuu wa maandamano, kwa sababu ya vitendo vyake vya ufisadi vilivyochangia watu kuingia mitaani katika miji 99 nchini Urusi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alexei Navalny alikamatwa Jumapili