Brazil: Kampuni ya ndege yailipa dola milioni 1.3 kwa kabila la Caiapó

Moja wa viongozi wa kijadi wa kabila la Caiapó
Image caption Moja wa viongozi wa kijadi wa kabila la Caiapó

Moja ya mashirika makubwa ya ndege nchini Brazil liitwalo Gol, limekubali kulipa dola milioni 1.3 kwa kabila moja ikiwa ni kulipia gharama za kuharibu eneo lao wakati ndege ya kampuni hiyo ilipoanguka katika eneo la kabila hilo zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Ndege hiyo ya kampuni binafsi ilianguka Kaskazini mwa Brazil mwaka 2006 na kutua katika eneo la kabila la Caiapó.

Image caption Timu ya uokoaji ilikumbana na changamoto kubwa kuokoa watu katika msitu huu mkubwa

Viongozi wa kabila hilo wanasema kuwa walilazimika kutengeneza makazi mapya sehemu za pembeni baada ya ndege hiyo kusababisha uharibifu mbaya wa mazingira, huku zaidi ya watu 150 wakifariki katika tukio hilo.