Watu 11 wauawa kwenye shambulio Yemen

Ni kawaida kwa matukio kama haya kutokea eneo hili
Image caption Ni kawaida kwa matukio kama haya kutokea eneo hili

Serikali ya Yemen imesema watu 11 waliuawa katika shambulio la kujitoa muhanga kwenye uwanja mmoja Kusini mwa nchi hiyo.

Maofisa wanasema kuwa gari dogo likiwa na vilipuzi, liliendeshwa mpaka kwenye uwanja wa serikali wa al-Houta uliokuwa na mkusanyiko wa watu.

Baadhi ya watu waliokuwa wamevalia mavazi ya kijeshi walitoka kwenye gari hilo na kuanza kushambulia raia na kisha bomu kwenye gari hilo lililipuka.

Shambulizi hili linatajwa kufanywa na kundi la Islamic State ambalo mpaka sasa hawajatoa tamko lolote.