Ahmed Kathrada alikuwa mtu wa aina gani?

Kathrada

Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi Ahmed Kathrada amefariki mjini Johannesburg.

Kathy, kama alivyojulikana kwa umaarufu alikuwa mojawapo ya marafiki wa karibu wa Nelson Mandela.

Lakini sio hilo tu, alikuwa pia mwanaharakati wa kutetea haki za binaadamu.

Kama Mandela, alifungwa kwa miaka 27 kwa kupinga utawala wa mtu mweupe kufuatia kesi maarufu mnamo 1963 ya Rivonia.

Alikuwa mtoto wa nne kati ya watoto sita waliozaliwa katika jimbo la kaskazini magharibi lililokuwa linajulikana kama Western Transvaal.

Akiwa na umri wa miaka 12 alijiunga kuwa mwanachama wa tawi la vijana la chama cha kikomunisti - the Young Communist League na baadaye alijiunga na chama cha Transvaal Indian Congress.

Kathrada alikamilisha shahada za historia, kuhusu masuala ya uhalifu na siasa za Afrika katika chu kikuu cha Afrika kusini, akiwa gerezani katika kisiwa cha Robben, na gereza la Pollsmoor .

Maafisa wa utawala wa ubaguzi wa rangi hawakumruhusu yeye na wenziwe kujiendeleza kwa masomo ya baada ya kuhitimu shahada ya kwanza.

Mnamo Juni 2013 alipokuwa anamuonyesha rais wa Marekani Barack Obama gereza alimokuwa katika kisiwa cha Robben alisema, "Nilikaa miaka 17 na nusu katika gereza hili. Jambo kuu unalilokosa ni watoto. Unawatamani watoto."

Lakini hata kwa kufuata siasa za Kathy alipokuwa kiongozi wa chama cha ANC tangu kuachiwa kwake kutoka gerezani mnamo mwaka 1990, atakumbukwa zaidi aliposoma wasifu wa Nelson Mandela katika mazishi yake mnamo 2013.

Alisema, ' nimempoteza Kaka, na kuna pengo kubwa katika maisha yangu sijui nimgeukie nani'.

Kathrada alikuwa na miaka 87.