Wanafunzi wa Nigeria washambuliwa India

Wanafunzi kutoka Afrika mara kwa mara hulalamikia tuhuma za kubaguliwa na wenyeji Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanafunzi kutoka Afrika mara kwa mara hulalamikia tuhuma za kubaguliwa na wenyeji

Waziri wa mambo ya nje wa India Sushma Swaraj, ameomba kufanyika kwa uchunguzi kufuatia tuhuma za kushambuliwa kwa Waafrika katika jimbo la Uttar Pradesh.

Wanafunzi wane kutoka Nigeria wanauguza majeraha baada ya kushambuliwa.

Msichana raia wa Nigeria anaarifiwa kutekwa na Waafrika wengine kushambuliwa hapo jana wakati wa maandamano ya kupinga kifo cha mvulana mmoja raia wa India katika mji wa Noida yaliyokumbwa na ghasia.

Inahofiwa mvulana huyo alipewa madawa ya kulevya kupita kiasi.

Waafrika ndio wanaotuhumiwa kwa uuzaji madawa hayo, na raia watano wa Nigeria walikamatwa kuhusiana na kisa hicho lakini wakaachiliwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi.

Raia wa Nigeria walishambuliwa siku ya Ijumaa katika mji huo kwa kutuhumiwa za kula watu.

Bw Sharawaj amesema waziri mkuu wa jimbo la Uttar Pradesh amemhakikishia kwamba uchunguzi huru utafanywa kuhusu visa vya kushambuliwa kwa wanafunzi hao.

Polisi wamewakamata watu watano, kwa mujibu wa taarifa kwenye vyombo vya habari India.

Kulishuhudiwa mashambulio kadha dhidi ya Waafrika mwaka jana katika mji mkuu Delhi.

Baadhi ya afisi za kibalozi za mataifa ya Afrika ziliilalamikia rasmi serikali ya India baada ya wanafunzi kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushambuliwa katika miji mbalimbali India.

Mada zinazohusiana