Mikebe ya Coca Cola yagunduliwa kuwa na kinyesi cha binadamu

Coca Cola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Coca Cola

Polisi wameanzisha uchunguzi wa kile kilichoonekana kuwa kinyesi cha binadamnu, kupatikana kwenye mikebe ya kujazwa soda iliyowasilishwa kwa kiwanda cha Coca Cola huko Ireland kaskazini.

Shughuli za usiku katika kiwanda cha Lisburn zilivurugwa wiki iliyopita wakati mashinde zilikwama.

Kampuni hiyo ilisema kuwa kisa hicho hakikuathiri vinywaji vyovyote ambavyo kwa sasa viko sokoni.

Polisi wanachunguza ripoti kuwa mikebe mingi huenda ilichafuka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Coca-Cola ina kiwanda kikubwa huko Lisburn
Haki miliki ya picha Albert Bridge
Image caption Kiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, Lisburn

Msemaji wa Coca-Cola amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifahamu kisa hicho cha mikebe mitupu katika kiwanda cha Knockmore.

"Tatizo hilo lilitambuliwa mara moja na bidhaa zote zilizoathirika kuzuiwa na haziwezi kuuzwa. Hiki ni kisa kilicho kando na hakiathiri biddaa zozote zilizo sokoni."msemaji wa Coca Coa alisema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii