Unawafahamu waliopinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini?

Unawafahamu waliopinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini? Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Unawafahamu waliopinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini?

Kufuatia kifo cha mwanaharakati wa kupinga serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Amhed Kathrada, sasa kuna watu wawili tu waliohukumiwa kifungo cha maisha kenye gereza la Rivonia mwaka 1964 walio hai, kwa kupinga ubaguazi wa rangi nchini humo.

Dennis Goldberg mwenye umri wa miaka 83, anaendelea kuzungumzia siasa za Afrika Kusini. Aliiambia BBC kuwa Kathrada hakuwa tu rafiki bali ndugu. Anasema kuwa walitaabika pamoja.

Andrew Mlangeni ,mwenye umri wa miaka 91 pia yeye yuko hai. Alihudumu kama mbunge wa kwanza nchini huo kwenye serikali iliyochagulia kidemokrasia kutoka mwaka 1994 hadi mwaka 1999.

Nelson Mandela aliaga dunia mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95. alihudumu kama rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia mwaka 1994.

Walter Sisulu aliaga dunia mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 90. Alikuwa makamu wa rais wa chama cha ANC toka mwaka 1991 hadi mwaka 1994.

Govan Mbeki, alifariki mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 91. alihudumua katika bunge la juu nchini Afrika Kusini toka mwaka 1994 hadi mwaka 1999. Mwanawe Thabo Mbeki alimrithi Mandela kama rais.

Raymond Mhlaba aliaga dunia mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 85. Alihudumu kama mwenyekiti wa chama cha South African Communist Party na pia alihuduma kama balozi wa Afrika Kusini nchini Rwanda na Uganda.

Elias Motsoaledi alifariki akiwa na umri wa miaka 69 siku moja kabla ya Mandela kuapiswa kuwa rais.