Mapigano kusitishwa Syria kunusuru raia

Wananchi wa Syria wakihama makazi yao kutokana na vita
Image caption Wananchi wa Syria wakihama makazi yao kutokana na vita

Kusitishwa kwa mapigano kunatarajiwa kufikiwa leo nchini Syria, ili kuruhusu kuondolewa kwa wananchi ambao wapo katika sehemu za hatari kwenye miji minne tofauti.

Chini ya makubaliano yaliyosainiwa na Qatar na Iran, wananchi wa miji hiyo ambayo inazungukwa na waasi ikiwemo Foah na Kefraya, wataondolewa katika maeneo hayo na kwenda kuishi katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali ya Damascus, Madaya na Zabadani.

Zoezi la awali la kuwaondoa wananchi katika maeneo ya hatari lilikwama miezi mitatu iliyopita kutokana na waasi kuzuia sehemu muhimu ambazo wangeliweza kuzitumia kupitia.