Trump abadili utaratibu wa Obama kukabiliana na joto duniani

Trump pia amewahi kupinga huduma ya afya ya Obama
Image caption Trump pia amewahi kupinga huduma ya afya ya Obama

Rais wa Marekani Donald Trump ametumia mamlaka yake kutengua utaratibu uliowekwa na mtangulizi wake Barack Obama, katika kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Trump amesema agizo la uhuru wa nishati ni mwanzo wa kipindi kipya cha uzalishwaji wa nishati.

Pia imefutilia mbali mahitaji yote ambayo maafisa wa serikali huyazingatia juu ya matokeo mabaya ya sheria yoyote mpya.

Akiungwa mkono na wachimbaji wa makaa ya mawe, Trump amesema italeta ajira.

Wachambuzi hata hivyo wamedokeza kuwa nishati mbadala zinaajiri watu wengi zaidi kuliko makaa ya mawe.