Ndege ya Peru yenye abiria 141 yashika moto
Huwezi kusikiliza tena

Ndege ya Peru iliyowabeba abiria 141 yashika moto

Ndege moja ya shirika la ndege la Peru, Peruvian Airlines, iliyokuwa imewabeba wabiria 141, imeshika moto baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Jauja, katika milima ya Andes.

Shirika hilo la ndege limesema wote waliokuwa ndani wameokolewa salama na hakuna aliyepata majeraha.

Ndege hiyo iliteleza na kutoka nje ya njia inayotumiwa na ndege kupaa na kutua.

Wazima moto walifanikiwa kuuzima moto huo.

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa hicho.

Mada zinazohusiana