Mwanamume aliyetoweka apatikana akiwa amekufa ndani ya chatu Indonesia

Mwanamume aliyetoweka apatika ndani ya chatu Indonesia Haki miliki ya picha West Sulawesi Police
Image caption Mwanamume aliyetoweka apatika ndani ya chatu Indonesia

Mwanamume mmoja nchini Indonesia ambaye alikuwa ametoweka amepatikana akiwa amekufa ndani ya tumbo la chatu, kwa mujibu wa polisi.

Akbar alitoweka siku ya Jumapili katika kisiwa cha Sulawesi, baada ya kuondoka nyumba akienda kuvuna mawese

Wakati nyoka huyo ambaye aliripotiwa kuwa na urefu wa mita saba alipopasuliwa tumbo, mwili wa mwanamume huyo ulipatikana ndani.

Chatu hunyonga na kisha kimeza myama yeyote ambaye anataka kumla.

Hata hivyo si kawaida kwa chatu kumla binadamu, lakini kuna visa vya chatu kuwameza watoto na wanyama.

Haki miliki ya picha West Sulawesi Police
Image caption Mwanamume aliyetoweka apatika ndani ya chatu Indonesia

Mashura ambaye ni msemaji wa polisi katika mkoa wa Sulawesi Magharibi aliiambia idhaa lugha ya Indonesia ya BBC, kuwa wanavijiji waliripoti kwa polisi kuwa Akbar amekuwa hajaonekana kwa muda wa sa 24.

Kisha polisi walianza kumtafuta na kumpata chatu huyo karibu na shamba la mawese la familia.

Baada kumkosa wanakijiji walimuoa chatu ambapo wakashuku kuwa huenda amemmeza Akbar. Wakati tumbo la chatu huyo lilipofunguliwa Akbar alikuwa ndan

Mada zinazohusiana