Samsung yazindua simu mpya ya Galaxy S8 iliyoboreka zaidi

Galaxy S8+
Image caption The Galaxy S8+ has a longer screen than last year's S7 Edge but is a smaller handset

Simu mpya za zinazotajwa kuwa zilizoboreka zaidi zinazinduliwa na kampuni ya Samsung.

Skrini za simu za Galaxy S8 na ya ile iliyo kubwa kidigo ya Galaxy S8+, ni kubwa licha ya siku zenyewe kuwa ndogo kuliko zile za mwaka uliopita za S7 na S7 Edge.

Wakati huu simu hizo zote zina skrini zilizojipinda hadi pembeni mwa simu.

Uzinduzi huo unafuatia kufeli kwa simu aina ya Note 7 ambayo ilirushwa mara mbii kufuaiua visa vya kuwaka moto.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini ilidai kuwa betri ndiyo ilikuwa na tatizo.

Kampunia hiyo pia imekuwa ikichunguzwa kwa madai kuhusika kwenye ufisadi nchini mwake.

Haki miliki ya picha Samsung
Image caption Samsung ilifanya uzinduzi katika miji ya London na New York

Siku ya Galaxy S8 inatajwa kuwa muhimu zaidi kuwai kuzinduliwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Simu hiyo inatajwa kuwa bora, lakini Samsung itahitaji kujitahidi ziadi ili kuepuka kasoro uliyokumba simu ya Note 7.

Simu hiyo itatolewa rasmi tarehe 21 mwezi Aprili mwaka huu.

Galaxy S8 itauza dola 856 nayo S8+ itauzwa dola 968.