Bendera ndefu India yabadilishwa baada ya kuchanika kwa upepo

Inasemekana kuwa bendera hii iliwekwa kwa haraka
Image caption Inasemekana kuwa bendera hii iliwekwa kwa haraka

Bendera ndefu zaidi huko India ambayo mnara wake upo juu ya mpaka wa Pakistan inabadilishwa kwa mara ya nne sasa baada ya kuendelea kuchanika kwa upepo.

Bendera hiyo ya taifa iliyo na urefu wa mita 600, ilipandishwa mwezi uliopita katika ukanda mkuu wa Wagah inayokatisha katika nchi hasimu ya jirani.

Mbadala umebidi kutafutwa kwasababu sheria za India zinasema bendera iliyoharibika haiwezi kupeperushwa.

Bendera hiyo iliwekwa hasa ili ionekane kutoka mji wa Pakistan ya Lahore yenye umbali wa kilomita ishirini.