Kumbe sokwe sio wapenzi wa muziki

Utafiti wa awali ulionyesha kuwa sokwe hupenda sana kusikiliza muziki
Image caption Utafiti wa awali ulionyesha kuwa sokwe hupenda sana kusikiliza muziki

Utafiti uliofanyika Uingereza na Marekani umegundua kuwa sokwe wakubwa na jamii nyinginezo sio wapenzi wakubwa wa muziki.

Utafiti huo unapingana na imani za walio wengi kuwa kupiga muziki maeneo ya hifadhi za wanyama huwafurahisha.

Watafiti hao walipiga muziki ambao unasemekana kupendwa na sokwe ungewafanya kufanya ni aina gani ya muziki wanaoupenda ikiwemo miondoko ya pop na nyinginezo.

Matokeo yake sokwe hao hawakuonyesha wamevutiwa haswa na aina gani ya wimbo, sio wa Ludwig van Beethoven ama Justin Bieber.

Katika tafiti za awali zinaonyesha sokwe huvutiwa na muziki wa taratibu zaidi ambapo unapingwa na utafiti wa sasa.