Shambulio la bomu laua maafisa Iraq

Mashambulizi kama haya yamekua yakitokea mara kwa mara Iraq
Image caption Mashambulizi kama haya yamekua yakitokea mara kwa mara Iraq

Maafisa wa Iraq wamesema watu wasiopungua 15 wameuawa katika mashambulizi ya bomu kwenye lori kusini mwa mji mkuu, Baghdad.

Zaidi ya watu 45 wanasemekana kujeruhiwa.

Gari hilo lililipuliwa katika kituo cha ukaguzi cha Polisi na miongoni mwa waliouwawa ni baadhi ya maafisa.

Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo lakini IS imekua ikifanya mashambulizi kama haya mara kwa mara baada ya kupoteza maeneo waliokua wakishikilia sehemu mbalimbali za Iraq.