Harusi 'ya Game of Thrones' yafanyika Marekani

Game of Thrones Haki miliki ya picha Katherine Elena Photography

Mashabiki sugu wa mwendelezo wa filamu za Game of Thrones waliamua kupiga hatua zaidi katika ushabiki wao kwa kufanya harusi ambayo iliiga filamu hiyo.

Makala mpya ya filamu hizo itatolewa katika kipindi cha miezi saba ijayo.

Mpiga picha Katie Lee anasema aliamua kuchukua hatua hiyo kujikumbusha kuhusu filamu hizo azipendazo sana.

"Nilijua kwamba lingekuwa jambo ngumu kufanikisha, nikiwa bado nahakikisha kwamba inakuwa harusi ya kufana," aliambia BBC.

Kulikuwa hata na mbweha - mbwa aliyepambwa kufanana na mbweha - kukamilisha muonekano wa Game of Thrones.

Haki miliki ya picha Katherine Elena Photography

Katie alihamasishwa zaidi na wahusika awapendao zaidi Daenerys Targaryen na Sansa Stark.

Haki miliki ya picha Katherine Elena Photography

Erin Foley aliyehusika katika mitindo na mavazi katika harusi hiyo anasema ndiyo yake aliyoifurahia zaidi na kwamba anajivunia pongezi ambazo amekuwa akipokea.

Haki miliki ya picha Lindsay Pizzuti
Image caption Lindsay Pizzuti alihusika katika kupamba nywele za bi harusi na bwana harusi
Haki miliki ya picha Katherine Elena Photography

Bila shaka, Game of Thrones haiwezi kukamilika bila mbweha.

"Nilitaka sana kuongeza mbweha," anasema Katie.

"Nilijua ingeboresha picha za harusi zaidi."

Walimtafuta mbwa kwa jina River katika kituo cha kutunza mbwa walioteswa na wamiliki wao na kutelekezwa.

Haki miliki ya picha Katherine Elena Photography

Harusi hiyo ilifanyika katika jumba la Smithmore ambalo linapatikana katika shamba la eka 121 katika mlima wa Blue Ridge, mashariki mwa Marekani.

Keki ilikuwa na sifa za zimwi, kwa heshima ya Daenerys, Mama wa Mazimwi.

Haki miliki ya picha Katherine Elena Photography

Mada zinazohusiana