Raia 28 wa Uchina wakamatwa Uganda

Rais 28 wa China wakamatwa Uganda
Image caption Rais 28 wa China wakamatwa Uganda

Maafisa wa uhamiaji nchini Uganda wamevamia makao ya kampuni moja ya ujenzi ya China, na kuwakamata raia 28 wa Uchina kwa madai kuwa wanaishi na kufanya kazi nchini humo kinyume na sheria.

Baadhi ya raia hao wa China walijifungia ndani ya viumba vyao, kwa kuhofia kukamatwa.

Karibu watu 16 walikamywa katika kambiayao kuu iliyo kijiji cha Kyebando, mashariki mwa Uganda, huku wengine 22 wakikamatwa kwenye timbo moja la mawe.

Kampuni hiyo ya China Railway, ilikuwa imeshinda zabuni ya kujenga barabara ya karibu kilomita 100 eneo hilo.

Maafisa hao wa uhamiaji walikuwa wameandamana na wenzao kutoka kwa halmashauri ya barabara ya Uganda wakati wa oparesheni hiyo.

Makampuni ya kichina yamekuwa wawekezaji wakubwa barani Afrika, lakini yamelaumiwa kwa kushindwa kuwapa kazi wenyeji au kuwatendea vibaya.