Trump kukutana na rais wa China Xi Jinping wiki ijayo

Trump (kushoto), Xi Jinping Haki miliki ya picha AP
Image caption Trump (kushoto), Xi Jinping

China imetanagaza tarehe ambayo rais wa nchi hiyo Xi Jinping, atasafiri kuenda Marekani kukutana na mwenyeji wake Rais Donald Trump.

Wawili hao watakutana katika eneo la starehe linalomilikiwa na Trump la Mar-a-Lago, huko Florida tarehe 6 na 7 Aprili.

Biashara itakuwa ajenda kuu kwa viongozi hao wa mataifa makubwa zaidi kiuchumi duniani pamoja na suala la Korea Kaskazini.

Uhusiano ulianza kuwa mbaya wakati Trump alipokea simu kutoka kwa rais wa Taiwaa lakini ukaboreka tena wakati Trump alidhibitisha sheria ya China moja.

Sera hiyo ya muda mrefu inasema kuwa kuna serikali moja tu ya China, jambo ambalo Tump amekuwa akilipinga hapo awali.

China inaitaja Tiwan kama mkoa wake uliojitenga na kutoa pingamizi kali baada ya mawasiliano hayo ya simu.

Bwana Trump alondoa msukosuko kati ya China na Marekani baada ya kumpigia simu bwana Xi na kuunga mkono sera ya China moja.

"Yalikuwa ni mazungumzo mazuri, tulikuwa na mazungumzo mazuri usiku uliopita na tulizungumzia masuala kadha, yalikuwa ni mazungumzo marefu." alisema Trump.

Xi atakuwa kiongozi wa pili kuzuru Marekani baada ya ziara ya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.