Mwili wa Kim Jong-nam kusalimishwa kwa Korea Kaskazini

Mwili ya Kim Jong-nam kusamishwa kwa Korea Kaskazini Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwili ya Kim Jong-nam kusamishwa kwa Korea Kaskazini

Malaysia imesema kuwa itasalimisha mwili wa ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini aliyeuawa kwenda Korea Kaskazini.

Waziri mkuu Najib Razak, anasema kuwa serikali ilikuwa imeidhindsha kusalamishwa mwili wa Kim Jong-nam.

Bwana kim aliuawa kwenye uwanja wa ndege Kuala Lumpur na kemikali kali mwezi uliopita.

Mauaji hayo yaliasababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya Malaysia na Korea KaskaziniMalaysia imesema kuwa itasalimisha mwili wa ndugu wa kambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini aliyeuawa kwenda Korea Kaskazini.

Waziri mkuu Najib anasema kuwa raia 9 wa Malaysia ambao wamekuwa wakizuiwa kuondoka Korea Kaskazini, sasa wamepewa ruhusa wa kuondoka nayo Malaysia itawaruhusu raia wa Korea Kaskazizi kuondoka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim alionekana akiomba msaada baada ya kushambuliwa na kemikali

Malaysia haijailaumu Korea Kaskazini moja kwa moja kwa mauaji hayo, lakini kuna shaka kuwa Korea Kaskazini ilihusika.

Wachunguzi wa Malaysia walikuwa wameitaka Korea Kaskazini kusalimisha washukiwa watatu kati yao wakiwa kujificha kwenye ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia.

"Serikali inaamini kuwepo haki na uhuru wa nchi. Uchunguzi wa polisi wetu kwenye kisa hiki kibaya katika ardhi yetu utaendelea." Najib alisema.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia wameshtakiwa kwa mauaji ya Kim Jong-nam

"Nimeamuru kila hatua kuchukuliwa ili kuwaleta wale wote waliohusika kwenyr mauaji haya.

Wanawake wawili mmoja raia wa Vietnam na mwingine raia wa Indonesia wamekamatwa kwa mauaji ya Kim.

Wote wanasema walifikiri walikuwa wakiigiza katika mchezo wa televisheni.