Mwizi akwama kwenye dohani siku mbili Zimbabwe

Mwizi akwama kwenye dohani siku mbili Zimbabwe Haki miliki ya picha The chronicle/twitter
Image caption Mwizi akwama kwenye dohani siku mbili Zimbabwe

Mwanamume ambye anashutumiwa kwa kujaribu kuiba alikwama kwenye dohani (sehemu inayojengwa kwenye paa ya kutolea moshi) katika kituo kimoja cha huduma kwa vijana.

Andrea Zunga, alikwama kwa muda wa siku mbili kabla ya kuokolewa na wazima moto na kuchukuliwa na polisi, kwa mjibu wa gazeti la serikali la Chronicle.

Zunga, mwenye umri wa miaka 33 alionekana kama zombi wakati alitolewa kwenye dohani hiyo.

Hata hivyo bwana Zunga bado hajazungumzia shutuma dhidi yake.

Gazeti la the Chronicle na mashirika mengine ya habari yamekuwa yakiandika taarifa kuhusu kisa hicho.

Haki miliki ya picha ZCN/TWITTER
Image caption Mwizi akwama kwenye dohani siku mbili Zimbabwe