Bajeti ya mwaka 2017 na 2018 yasomwa Kenya

Polisi wakipiga doria nje ya bunge wakati wa kusomwa kwa bajeti
Image caption Polisi wakipiga doria nje ya bunge wakati wa kusomwa kwa bajeti

Bajeti ya Kenya ya mwaka 2017/2018, imesomwa leo kinyume na inavyosomwa kawaida mwezi Juni, kutokana na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwezi Agosti.

Waziri wa fedha Henry Rotich aliondoa kodi mahindi yanayoagizwa kutoka nje katika kipindi cha miezi minne ijayo.

Pia utengezaji wa dawa za kuua wadudu umeondolewa kodi pamoja na magari ya utalii yanayoundwa nchini Kenya.

Kama moja ya njia ya kuzuia uchezaji kamari, serikali imeongezea kodi sekta hiyo hadi asilimia 50 kutoka asilimia 7.5 ya awali.

Bajeti hii ndiyo ya mwisho ya serikali ya Jubilee katika muhua wake wa kwanza serikalini.

Ili kupunguza matumizi ya serikali, waziri wa fedha alitangaza kusimamishwa kuajiriwa kwa watu katika sekta za umma ijapokuwa katika sekta kama za elimu.

Image caption Ili kuhakikisha kuwa vijana wana ajira, serikali imetenga shilingi milioni 450 kwa kuboresha kiwanda cha Rivatex, na zingine milioni 250 kuboresha kiwanda cha maziwa cha New KCC.

Shilingi bilioni 2 zimetengwa kuwaajiri walimu, na zingine bilioni 4 kuwalipia mtihani wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nnemwaka 2017 na 2018.

Nazo serikali za kaunti zitapata jumla la shilingi bilioni 329.

Ili kuhakikisha kuwa vijana wana ajira, serikali imetenga shilingi milioni 450 kwa kuboresha kiwanda cha Rivatex, na zingine milioni 250 kuboresha kiwanda cha maziwa cha New KCC.

Shilingi bilioni 524.6 za bajeti hiyo zitatokana na mikopo kutoka nje na ndani ya nchi.