Trump aongeza mashambulizi zaidi dhidi ya Al Shabab

Trump anataja hatua hii kama chachu ya kuwamaliza wanamgambo hao haraka
Image caption Trump anataja hatua hii kama chachu ya kuwamaliza wanamgambo hao haraka

Rais wa Marekani Donald Trump ameliruhusu jeshi la nchi hiyo kuongeza mashambulizi zaidi nchini Somalia kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa Al Shabab.

Hii italifanya jeshi la Marekani kutumia nguvu zaidi sambamba na vifaa vya kisasa kupambana na wana mgambo hao, huku pia wakitoa usaidizi wa karibu kwa jeshi la Somalia.

Inatarajiwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani wataelekea nchini Somalia kwa ajili ya operesheni hii.

Al Shabab wameendelea kufanya mashambulizi yanayosababisha vifo kila kukicha nchini Somalia na hata katika nchi jirani ya Kenya.