Wanamgambo elfu mbili wa IS wauawa Iraq tokea Februari

IS bado ni tishio nchini Iraq
Image caption IS bado ni tishio nchini Iraq

Jeshi la Marekani limesema linaamini kuwa takriban wanamgambo elfu moja wa Islamic State wameuawa tokea kuanza kwa oparesheni ya kuwaondoa Magharibi mwa mji wa Iraq, Mosul.

Msemaji wa jeshi la Marekani linalounga mkono jeshi la Iraq, amesema kuwa walikuwepo wanamgambo takriban elfu mbili mwezi Februari.

Na kwa sasa wanaamini wamesalia pungufu ya nusu ya hao.

Pamekuwa na wiki ya mapigano makali mjini Mosul.

Sambamba na kuuawa kwa wanajeshi kutoka kila pande, pamekuwepo pia na taarifa za kuuawa kwa wananchi wengi.