Israel kujenga mji wa kwanza West Bank

Israel na Palestina zimekua zikiingia katika migogoro ya ardhi mara kwa mara
Image caption Israel na Palestina zimekua zikiingia katika migogoro ya ardhi mara kwa mara

Israel imesema kuwa kwa mara ya kwanza itajenga mji wake wa kwanza katika eneo la West Bank ikiwa ni zaidi ya miaka 20.

Ujenzi huo utakaofanyika karibia na mji wa Palestina wa Nablus ulithibitishwa katika kikao cha kamati ya ulinzi siku ya Alhamisi.

Itatumika kwa raia wa nchi hiyo ambao waliondoka Amona mji ambao mahakama inasema ulijengwa kimakosa katika ardhi ya Palestina.

Mwezi uliopita Rais Trump alitaka nchi hizo mbili kufikia muafaka kuhusu maeneo hayo mapema ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima.