Kim Jong-nam: Korea Kaskazini yawaachilia raia wa Malaysia

Mohd Nur Azrin Md Zin31 Machi 2017 Haki miliki ya picha European Photopress Agency
Image caption Miongoni mwa waliolerejea ni mwanabalozi wa Malaysia aliyekuwa akihudumu Korea Kaskazini Mohd Nor Azrin Md Zain (kati)

Raia tisa wa Malaysia waliokuwa wamezuiliwa Korea Kaskazini wamewasili nyumbani, baada ya mataifa hayo mawili kuafikiana na kumaliza mzozo wa kidiplomasia.

Mzozo ulizuka baina ya mataifa hayo mawili mwezi uliopita kutokana na kuuawa kwa Kim Jong-nam, ndiguye wa kambo wa Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpur.

Mataifa hayo yaliwazuia raia wa nchi pinzani kuondoka.

Malaysia pia imekubali kuachilia mwili wa Kim.

Kumekuwa na uvumi kwamba Pyongyang ilihusika katika mauaji ya Bw Kim.

Mwana huyo wa kwanza wa kiume wa Kim Jong-il anadaiwa kutoroka Korea Kaskazini baada ya kukosa kupatiwa uongozi wa taifa hilo kufuatia kifo cha babake.

Raia wa Malaysia walioruhusiwa kuondoka Korea Kaskazini walilakiwa na jamaa na wanahabari katika uwanja wa ndege wa 'Kuala Lumpur mapema Ijumaa.

Haki miliki ya picha European Photopress Agency
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Malaysia Anifan Aman (mwenye koti la waridi) akiwalaki raia waliorejea Kuala Lumpur

Miongoni mwa waliolerejea ni mwanabalozi wa Malaysia aliyekuwa akihudumu Korea Kaskazini Mohd Nor Azrin Md Zain, maafisa wa ubalozi na jamaa zao.

Mwanabalozi huyo alisema waliingiwa na wasiwasi sana serikali ya Korea Kaskazini ilipowaambia kwamba hawawezi kurejea nyumbani.

Walisafirishwa kwa ndege ya kibiashara iliyoendeshwa na maafisa wa jeshi la wanahewa la Malaysia.

Bw Kim aliuawa 13 Februari. Korea Kaskazini iliitaka Malaysia kuachilia mwili wake lakini ombi hilo likakataliwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bw Kim alikuwa nduguye wa kambo wa Kim Jong-un

Taarifa zinasema raia wote wa Korea Kaskazini nao wataruhusiwa kuondoka Malaysia, ikiwa ni pamoja na washukiwa wawili raia wa Korea Kaskazini waliokuwa wanasakwa na polisi wa Malaysia.

Shirika la habari la Japan Kyodo limesema watu wawili waliofanana na washukiwa wawili wanaotafutwa, walionekana kwenye ndege ya kuelekea Beijing ambayo ilikuwa imeubeba mweili wa Bw Kim Ijumaa.

Washukiwa hao wawili ni Hyon Kwang Song, katibu wa pili wa ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Kuala Lumpur, na Kim Uk Il, mfanyakazi wa shirika la ndege la Korea Kaskazini Air Koryo.

Haki miliki ya picha Kyodo/Reuters
Image caption Mwanamume wa kwanza kushoto anafanana na Kim Uk Il

Wawili hao walikuwa wamekatalia ndani ya ubalozi na walikataa kushiriki katika uchunguzi wa mauaji hayo.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Maafisa wa Korea Kaskazini na China wanaonekana katika uwanja wa ndege Beijing baada ya ndege iliyobeba mwili wa Kim kutua Ijumaa

O

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii