Mwili wa Kim Jong-un wawasili Korea Kaskazini

Mwili wa Kim ukiondolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwili wa Kim ukiondolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti

Mwili wa Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, umewasili nchini Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini ilikuwa imeomba kupewa mwili huo lakini haikuwa imesema ulikuwa ni wa nani.

Mwili huo ulitolewa kwa Korea Kaskazini kama sehemu ya makubaliano ambapo raia 9 wa Malaysia, waliizuiwa kuondoka Korea Kaskazini waliwasili nyumbani.

Nchi hizo mbili zimekuwa kwenyr mzozo wa kidiplomasia kufuatia mauaji ya Kim, kwenye uwanja wa Kuala Lumpur mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bwana Kim ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini

Kila nchi ilikuwa imewapiga marugufuku raia wa nchi nyingine kuondoka.

Raia watatu wa Korea Kaskazini wameruhusiwa kuondoka malaysia, kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa nchi hiyo.

Korea Kaskazini inashukiwa pakubwa kuhusika kwenye kifo cha bwana Kim, kwa kutumia kemikali akiwa uwanja wa Kuala Lumpur.

Haki miliki ya picha European Photopress Agency
Image caption Raia wa Malaysia wakaribishwa nyumbani
Haki miliki ya picha Kyodo/Reuters
Image caption Raia wa Korea Kaskazini wakiondoka Malaysia