Matumizi ya simu yalichangia vifo vingi kwa kusababisha ajali za barabarani Marekani

Matumizi ya simu yalichangia vifo vingi kwa kusababisha ajali za barabarani Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matumizi ya simu yalichangia vifo vingi kwa kusababisha ajali za barabarani Marekani

Kuongezeka kwa kasi vifo vya watu wanaosafiri kwa miguu nchini Marekani, kumetajwa kutokana na watu kutumia simu zao wakati wakiendesha magari au wanapovuka barabara.

Halmashauri inayohusika na usafri wa barabarani nchini Marekani inakadiria kuwa wasafiri 6000 wanaotembea walifariki mwaka 2016 ikiwa ndiyo idasi kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 20.

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita vifo vimeongezeka mara nne zaidi.

Ripoti inasema kuwa masuala kadha yamechangia ikiwemo matumizi ya simu za mkononi.

Suala la hivi punde ambao limechangia kuongezeka kwa vifo vya watu wanaotembea ni matumizi ya simu za smartphone na watumiaji wote wa barabara.

Sababu zingine ni pamoja na watu wengi kumiliki magari kufuatia kuboreka kwa uchumi, bei ya chini ya petroli na watu wengi kutembea kama njia ya kufanya mazoezi.

Pombe nayo imelaumiwa kwa kuchangia, huu asilimia 34 ya wasafiri wa miguu na asilimia 15 na madereva wakihusika kwenye ajali mbaya wakiwa wamelewa.

Ripoti hiyo imetokana na takwimu kutoka majimbo yote kwa miezi 16 ya kwanza ya mwaka 2016.