Kiti chenye mfano wa uume chazua mjadala Mexico

Kiti kilicho na mfano wa uume chazua mjadala Mexico Haki miliki ya picha YouTube
Image caption Kiti kilicho na mfano wa uume chazua mjadala Mexico

Wakati aina mpya ya kiti kilionekana ghafla ndani ya treni kwenye mji mku nchini Mexico, Mexico City, kiti hicho kilitajwa kuwa cha kuchukiza na cha aibu.

Kiti hicho kina mfano wa uume na kifua kilichotengenezwa kuashiria udhalilishaji wa kingono wanaopitia abiria wanawake.

Kiti hicho si cha kudumu , lakini ni sehemu ya kampeni iliyoziduliwa na wanawaka wa Umoja wa Mataifa, yenye lengo la kuangazia udhalilishaji wa kingono kweney usafiri wa umma

Kwenye video iliyochapishwa na kutazamwa mara 700,000 muda siku kumi zilizopita, bbadhi ya watu waliipongeza huku wengine wakisema kuwa haikuwatendea vyema wanaume.

Sekta ya usafiri wa umma kwa njia ya treni nchini Mexico imekuwa na historia mbaya kutokana na tatizo la usalama wa wanawake.

Haki miliki ya picha YouTube
Image caption Kiti kilicho na mfano wa uume chazua mjadala Mexico

Mwaka 2014 kampuni moja ya Uingereza ilindesha utafiti kuhusu udhalilishaji kwenye sekta ya usafiti wa umma kote duniani.

Kwa udhalilishaji wa kingono kwa njia ya maneno na kwa kimwili, sekta ya usafiri wa umma nchini Mexico ilichukua nafasi ya kwanza.

Kwa miaka mingi mji wa Mexico City, umejaribu njia tofauti za kuwawezesha wanawake kuhisi kuwa salama.