Msusi mwenye umri wa miaka 93 astaafu

Msusi mwenye umri wa miaka 93 astaafu Haki miliki ya picha Bc
Image caption Msusi mwenye umri wa miaka 93 astaafu

Msusi mmoja amestaafu baada ya kufanya kazi kwenye duka moja la urembo kwa miaka jumla ya 72.

Kathleen Privett mwenye umri wa miaka 93, ameamua kufunga duka hilo lililo Drayton, Portsmouh, ambalo lilianzishwa na babaka mwaka 1945.

Bi Privett, anasema awakosa wateja ambao mara nyingi hufichua siri zao za kimaisha.

Baada ya kumpoteza mumeme akiwa na umri wa miaka 28, alichua usukani baada ya baba yake kufariki mwaka 1962.

Image caption Msusi mwenye umri wa miaka 93 astaafu

Alifanya kazi na bintiye Barbara Ecana ambaye sasa ana umri wa miaka 70 ambaye naye ameemua kustaafu.

Bi Privett anasema kuwa amefanya kazi miaka hiyo yote kwa sababu alikuwa akiipenda kazi yake.

"Ni wateja ambao hufanikisha, vitu ambavyo wao hukuambia ambavyo ni vya siri." alisema Privett.