Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa

Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mali ya Ivanka Trump na mumewe yafichuliwa

Ikulu ya Marekani, imetoa maelezo kuhusu mali ya binafsi ya watu waliomo katika serikali ya Rais Donald Trump.

Mali hiyo imedhihirishwa kama sheria inavyoelekeza, na inaonyesha kuwa mtoto wa rais wa kike, Ivanka pamoja na mumewe Jared Kushner, wana takriban dola milioni 240 na 740 mtawalia.

Hii ni pamoja na hisa kwenye hoteli ya Trump International, ambazo zilimpa Ivanka kati ya dola milioni 1 na milioni 5 mwaka uliopita.

Ufichuzi huo wa mali pia unaonyesha mishahara na watu wengine wa vyeo vya juu uongozini.

Nyaraka zilizotolewa pia zilionyesha mali wakati wakianza kuifanyika kazi serikali na kabla la mali yoyote kuuzwa

Ikulu ya White House inajaribu kuonyesha kuwa watu katika serikali ya Trump wanajiweza, na inasema watu hao wamejitolea sana kwa kukubali kutumika serikalini.

Watu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu walio kwenye baraza la mawaziri la bwana Trump wana jumla ya mali ya dola bilioni 12.