Afrika Kusini yapata waziri mpya wa fedha

Malusi Gigab Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Malusi Gigab

Waziri wa Fedha mpya wa Afrika Kusini, Malusi Gigaba, amesema wakati umefika wa kubadilisha sana uchumi.

Amesema, kwa muda mrefu Afrika Kusini inahodhiwa na wawekezaji wa nchi za nje.

Pia amekiri kwamba kutolewa kazini kwa waziri aliyemtangulia hapo jana, Pravin Gordhan, kumeigawa nchi.

Bwana Gordhan anayeheshimiwa kimataifa, alipotolewa kazini ghafla, katika mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyofanya Rais Jacob Zuma, kulizuka malalamiko kutoka kwa watu wengi, pamoja na makamu wa rais, Cyril Ramaphosa, na wanasiasa mashuhuri katika chama tawala cha ANC.

Vyama vya upinzani, vinasema, Bwana Gordhan aliondolewa, kwa sababu alimzuwia Rais Zuma na washirika wake, wasipate nafasi ya kufikia mali ya taifa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bwana Gordhan alifutwa hali iliyozua kushuka kwa masoko ya hisa