Mwanamuziki Bob Dylan akubali kuchukua tuzo la Nobel

Bob Dylan akubali kuchukua tuzo la Nobel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bob Dylan akubali kuchukua tuzo la Nobel

Mwanamuziki mashuhuri Bob Dylan hatimaye amekwenda kuichukua zawadi yake ya Nobel kuhusu maswala ya fasihi, zaidi ya miezi sita tangu alipotangazwa mshindi.

Wanachama wa shirikisho lililotoa tuzo hiyo ya huko Sweden, wamethibitisha hilo baada ya kukutana na mwanamuziki huyo kabla ya kufanya tamasha lake la jana mjini Stockholm.

Kinyume na utamaduni wa mbwembwe unaoandamana na utoaji wa tuzo kama hilo, hamna maelezo yoyote ya ziada yaliyotolewa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bob Dylan mwenye umri wa miaka 75, hakuhudhuria sherehe rasmi za awali za tuzo hilo zilizofanyika Decemba mwaka jana.

Bob Dylan mwenye umri wa miaka 75, hakuhudhuria sherehe rasmi za awali za tuzo hilo zilizofanyika Decemba mwaka jana.

Sasa amepewa mda wa mpaka tarehe 10 Juni ambapo anatakiwa kutoa hotuba yake kwa mujibu wa taratibu zinazoambatana na tuzo za Nobel , la sivyo hatakabidhiwa fedha zinazoambatana na zawadi hiyo zipatazo dolla laki 9.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii